Maafisa wanne wa usalama kutoka eneo Laikipia Magharibi wanapokea matibabu katika hospitali ya Sipili Baada ya kambi yao kuvamia na wahalifu wanaodaiwa kuwa wezi wa mifugo.
Akidhibitisha kisa hicho Naibu Kamishna wa eneo hilo la Laikipia Magharibi Hezron Nyamberi amesema kuwa wezi hao walivamia kambi hiyo iliyoko karibu na Hifadhi ya msitu ya Laikipia na kuanza kufyatua marisasi.
Haya yanajiri baada ya waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i kuamrisha wafugaji hao ambao wamekuwa wakilisha mashamba ya watu kuhama kaunti hiyo ya Laikipia Jambo ambalo hawajalitekeleza.
Leave a Comment