News/Habari

LAMU: WANAMGAMBO BADO WAPO WAPO SANA!!!

Written by admin
Mtu mmoja zaidi ameuawa kufuatia shambulizi la watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab katika eneo la Bobo-Hindi kaunti ya Lamu.

Kulingana na ripoti za polisi, watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi hilo haramu walimteketeza mwanamume huyo kwa jina John Moji kiasi cha kutotambulika na aadaye kubomoa nyumba yake katika tukio hilo la usiku wa kuamkia leo.

Akithibitisha kisa hicho, mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi Eliud Kinuthia amesema Moji alifariki akiwa amefungwa mikono yake nyuma ya mgongo wake, tukio sawa na namna watu wengine 6 walivyoouawa alfajiri ya jana.

Kinuthia hata hivyo amewapongeza polisi kwa hatua yao ya haraka ya kulilinda eneo hilo kabla ya washukiwa hao kutekeleza mauaji zaidi.

About the author

admin

Leave a Comment