Maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai DCI wamewakamata maafisa wawili wa magereza kuhusiana na kisa cha kuangamizwa kwa mfungwa Simon Nduro wa gereza la Naivasha.
Kulingana na DCI washukiwa hao Sergeant Dennis Wandati Masibo na Obadiah Meriti Lansika wa cheo cha konstebo alias Masai wanatarajiwa kuwalishwa mahakamani kuhusiana na kifo cha cha Nduro juni mwaka jana.
Haya yanakuja baada ya uchunguzi wa maiti yake kuonyesha kuwa aliaga dunia kutokana na majeraha aliyopata kutokana na kichapo cha maafisa hao wa magereza.
Ripoti ya mpasuaji wa serikali Titus Ngulungu ilitofatiana na ile ya idara ya mahakama ilidai kuwa mwendazake aliangamia kutokana na ugonjwa wa asthma.
Mamake mfungwa mwendazake Mary Njeri anaitaka idara ya DCI kufanya uchunguzi wake kikamilifu ili haki iaptikane.
Leave a Comment