News/Habari

MAHAKAMANI: KORONA YAHAIRISHA KESI YA GAVANA

Gavana wa kaunti ya Migori Okoth Obado
Written by admin

Kesi ya ufisadi inayomkabili gavana wa Migori Okoth Obado imehairishwa baada ya mshukiwa mmoja waliokuwa wameshtakiwa pamoja kuugua korona.

Hakimu Lawrence Mugambi ambaye alikuwa asikize kesi hiyo alifahamishwa kwamba mshtakiwa mmoja, Peninah Auma alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Mahakama ilikuwa imepanga kuskiza ushahidi dhidi ya gavana Obado, watoto wake wanne pamoja na washtakiwa wengine.

Hakimu ameagiza kesi hiyo itajwe kesho wakati ambapo mahakama itafahamishwa kuhusu hali ya afya ya mshtakiwa.

Huenda kesi hiyo ikaendelea Alhamisi wiki hii iwapo hali ya mshtakiwa itakuwa nzuri.

Mwaka uliopita gavana Obado pamoja na watoto wake walishtakiwa kwa kushirikiana kwenye ufisadi uliohusisha shilingi milioni 73.4 za kaunti ya Migori.

About the author

admin

Leave a Comment