News/Habari

Majambazi sugu wauawa Eldoret

Written by admin

Polisi mjini Eldoret wamewaua Majambazi wanne kwa kuwapiga risasi katika eneo la West karibu na kanisa la International Vision Centre IVC barabara kuu ya Eldoret- Uganda viungani mwa mji wa Eldoret.

Akithibitisha hayo Kamanda wa polisi Kaunti ya Uasin Gishu Johnstone Ipara amesema kuwa, maafisa wa polisi waliokuwa wakipiga doria katika eneo hilo walijaribu kusimamisha gari lililokuwa likienda kwa kasi na badala yake watu hao wakaanza kuwafyatulia maafisa hao risasi ambapo maafisa hao pia walilazimika kuwapiga risasi na kuwauwa wanne hao papo hapo. 

Ipara ametoa onyo kali kwa wale ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakaazi katika eneo hilo pamoja na wanaoshirikiana nao kuwa watakabiliwa kwa mujibu wa sheria akitaja kuwa wahalifu hao walipatikana na silaha hatari. Amewataka wale ambao wanamiliki silaha kupeleka katika kituo cha polisi kabla ya maafisa kuanzisha msako.

Ipara vilevile, amesema wahalifu haohao waliwahangaisha wakaazi mwaka uliopita katika mji wa Eldoret.

About the author

admin

Leave a Comment