Idadi ya watu wanaoishi na ulemavu ambao wamepata usaidizi kutoka idara kitaifa ya watu wanaoishi na ulemavu mwaka huu katika eneo bunge la Keiyo kaskazini kaunti ya Elgeyo Marakwet imepungua kwa asilimia 46.
Haya ni kwa mujibu wa Afisa kutoka idara hiyo Isaack Kalia ambaye amesema katika mwaka wa 2018 watu 28 walipata uzaidizi huo huku watu 13 wakipata uzaidizi mwaka huu.
Akiongea alipopeana vifaa vilivyogharimu shilingi elfu mia tatu mjini Iten, Kalia amesema jamii hiyo haikuweza kupewa uhamasisho wa kutosha kuhusu jinsi ya kupeana ombi la kupata vifaa hivyo.
“Ningependa kutoa shukranui kwa seerikali kuu kwa sababu ya kusaidia walemavu kujikimu kimaisha,hivi vifaa vimenunuliwa ili kuwasaidia walemavu , na kama kuna mtu amabaye angetaka kujitolea basi tunaomba atusaidie kwani bado kuna changamoto”Isaack Kalia amesema.
Beatrice Koech
Leave a Comment