News

Mbunge wa Subukia aapa kufuatilia kesi ya bwawa la Solai

Written by admin

Mbunge wa Subukia Samuel Gachobe amelaumu uamuzi uliotolewa na mahakama ya Naivasha, kwa kuwaweka huru watuhumiwa wa bwawa la Patel, kuhusiana na mkasa uliopelekea vifo vya watu arobaine na nane.

Akiongea na kituo hiki, Gachobe amesema kuwa uamuzi huo haukutolewa kwa njia ya haki, kwani wengi wa waathiriwa huishi maisha ya umaskini, tangu kutokea kwa mkasa huo, na hivyo wanapaswa kupewa fidia.

Aidha, kiongozi huyu ameongeza kuwa, Kama kiongozi wa eneo hilo atahakikisha waathiriwa wote wamepata haki yao kwa njia ya uwazi.

WARUKIRA.

About the author

admin

Leave a Comment