News/Habari

MICHEZO: Mataifa kulishwa wa Chuya

[Kushoto kwenda kulia] washambulizi wa Liverpool Salah, Firmino na Mane. Picha kwa hisani ya Premier League
Written by admin

Klabu ya Liverpool imekataa kumruhusu nyota wake raia wa Misri Mohamed Salah kwenda kuitumikia timu yake ya taifa katika mechi za mwezi ujao za kufuzu kombe la dunia.

Kwa mujibu wa Chama cha soka cha Misri sababu kubwa ya klabu hiyo kugoma kumruhusu Salah kucheza mechi hizo ni kwa sababu ya sharti la kutakiwa kukaa karantini kwa siku 10, mara atakaporejea kutoka Afrika.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa Klabu hiyo haitawaruhusu pia nyota wake raia wa wa brazil Roberto Firmino, Allison na Fabinho, kujiunga na timu ya taifa kwa sababu hizo hizo.

Vilabu vingine vya Ulaya vinaelezwa kutaka kuchukua hatua hiyo kwa wachezaji wao wanaotoka kwenye nchi zilizowekwa kwenye kundi la mataifa yenye hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya korona.

Hatua hiyo inaelezwa huenda ikaleta mzozo baina ya vilabu hivyo na vyombo vinavyoongoza soka vya mataifa wanakotoka wachezaji hao.

Mwezi uliopita Shirikisho la soka duniani (FIFA) lilifuta msamaha maalumu uliowekwa mwaka jana kwa ajili ya janga la corona, ulioruhusu vilabu kukataa kuwaruhusu wachezaji wake kwenda kwenye timu zao za taifa ikiwa kuna vikwazo vya kusafiri.

About the author

admin

Leave a Comment