News/Habari

MICHEZO: TUNISIA BINGWA!!

Written by admin

Tunisia ilihifadhi taji la bara Afrika katika mpira wa kikapu (FIBA Afrobasket) upande wa wanaume, baada ya kuwaangusha Ivory Coast pointi 78-75 jioni ya jana katika ukumbi wa Kigali nchini Rwanda.

Tunisia walinyakua robo mbili za mchuano wa kwanza 25-18, 22-16 na kuongoza kipindi cha kwanza alama 47-44.

Robo ya tatu na nne zilikuwa ngumu kwa Tunisia wakipoteza 18-25 na 13 -16, lakini uongozi huo haukotosha kuwapa Ivory Coast ushindi wakilemewa pointi 74-78.

Kwa jumla Tunisia wameshinda ubingwa wa Afrika mwaka 2011 mjini Antananarivo Madagascar na 2017 fainali zilizoandaliwa kwa pamoja na Tunisia na Senegal.


About the author

admin

Leave a Comment