Watoto watatu walio na umri wa miaka 4, 5 na 6 mtawalia, wameangamia kwenye moto uliozuka kwenye nyumba yao kule Turi Elburgon usiku wa kuakia leo.
Kulingana na ripoti ya polisi, baba ya watoto hao alikuwa ameenda dukani kununua maziwa wakati moto ulizuka kwenye nyumba yao.
George Omoso, amesema akiwa kwenye kituo hicho cha kibiashara ndipo alifahamishwa kuna moto kwake nyumbani, na aliporudi akapata watoto wamechomekea mle ndani.
Omoso amekuwa akilea watoto hao baada ya mkewe kumtoroka.
OCPD wa Molo Mwenda Muthamia anasema uchunguzi umeanzishwa kutambua kiini cha moto huo.
Maafisa kutoka serikali ya kaunti ya Nakuru wakiongozwa na Stephen Kung’u wamefika katika eneo la mkasa na kufariji familia hiyo.
Leave a Comment