Maafisa wa DCI wamemkamata jamaa anayedaiwa kumua mwanamke kwa kumrusha kutoka roshani ya chumba chao cha kulala kilicho katika jengo la Nyali Sunny Side, kaunti ya Mombasa.
Mshukiwa Suleiman Mayanja ambaye ni raia wa Uganda alipatikana katika maficho yake katika jengo la Nyali Cinemax.
Mayanja anadaiwa kuenda mafichoni baada ya kumrusha mwanamke huyo wa miaka 25 kutoka kwa roshani ya chumba chake cha malazi mida ya saa tisa asubuhi ya kuamkia Jumatatu.
Mlinzi ambaye alikuwa analinda jengo lile alisikia mayowe ya mwanamke kutoka hewani kabla kishindo kikubwa kusikika sekunde chache baadae.
Mlinzi huyo alipokaribia kile alichosikia kikianguka alipigwa na butwa kubwa kuona kuwa ulikuwa mwili wa mwanamke aliyekuwa nusu uchi. Mwili huo ulikuwa umezungukwa na dimbwi la damu.
Wasimamizi wa jengo hilo walipogundua kuwa mwili ule ulikuwa wa mwanadada aliyekuwa ameandamana na Mayanja usiku walienda hadi kwa chumba chake na kupata mlango ukiwa wazi na hakuna yeyote aliyekuwa mle ndani.
Inasemekana kwamba mshukiwa aliwasili nchini mnamo Septemba 1 na walikuwa wamejuana na mwanadada ambaye anadaiwa kuua kwa kipindi cha siku moja tu.
Leave a Comment