Shule ya upili ya Kambaa katika kaunti ndogo ya Lari kule Kiambu imefungwa kwa muda baada ya moto kuteketeza moja ya mabweni yake.
Mwenyekiti wa bodi simamizi wa shule hiyo Mukua Ngatia amesema kutokana na uharibifu uliotokea, walionelea heri kuwatuma nyumbani wanafunzi kwani haiwezekani kuwasetiri shuleni kwa sasa.
Ngatia amesema polisi wameanzisha uchunguzi wa kiini cha moto huo, akisema wazazi watajuzwa kuhusu lini shule hiyo itafunguliwa tena.
Moto huo uliteketeza bweni la orofa mbili ambalo hutumika na wanafunzi 200 kati ya 700 walio shuleni huo.
Leave a Comment