Maafisa wa haki za watoto katika kaunti ndogo ya Subukia wamemuokoa msichana wa miaka miwili, ambaye amekuwa akinajisiwa na babu yake mwenye umri wa miaka 72 katika Kijiji cha Kanyotu Subukia.
Akithibitisha kisa hiki OCPD wa kaunti ndogo ya Subukia Edward Imbwaga amesema kuwa hata baada ya wazazi wa mtoto huyo kufahamu kitendo hicho hawakuweza kupiga ripoti kwa maafisa wa polisi, kwani hawakutaka hatua yoyote iweze kuchukuliwa.
Aidha, Imbwaga amesema kuwa mamake mtoto huyo ameenda mafichoni baada ya kugundua kwamba habari kuhusu baba mkwe imeweza kuwafikia maafisa wa polisi.
Leave a Comment