News/Habari

Murang’a kufanya uamuzi mpya kuhusu miradi

Kang'ata kutathmini
Written by admin

Gavana wa Murang’a Irungu Kang’ata amesema Kituo cha Saratani kilichoanzishwa na mtangulizi wake Mwangi wa Iria kilikuwa mradi wa unaowajali watu kadhaa.

Kang’ata amesema hakuna mipango mwafaka ya kuanzisha kituo hicho katika Hospitali ya Murang’a Level Five na kuanza kufanya kazi na hivyo fedha za umma zingepotea.

Gavana huyo sasa amependekeza muundo mpya wa mradi huo utumike kushikilia vifaa vingine vya hospitali hiyo.

Jana, timu ya maafisa kutoka idara ya Fedha ilitembelea eneo hilo kwa tathmini kama ilivyoagizwa na gavana.

Afisa Mtendaji wa Fedha David Waweru pia amemwandikia Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Nancy Gathungu akimwomba aidhinishe timu kufanya ukaguzi wa miswada yote ambayo haijashughulikiwa katika kaunti.

About the author

admin

Leave a Comment