News/Habari

MURANG’A: WIZI WA KIWANGO CHA LAMI

Written by admin

Idara ya upelelezi wa jinai inafuatilia tukio ambapo Mwanamme mmoja amepoteza gari lake lililoharibika njiani mwendo wa saa nane Alfajiri.

Stephen Kamau alikuwa akielekea  Murang’a kutoka Maragua wakati aliliacha gari lake njiani mwendo wa saa kumi na moja asubuhi baada ya kukaa mle ndani kwa saa takriban tatu lilipoharibika na kwenda kutafuta makanika ila aliporejea hakulipata.

Kamau aliondoka kwa dakika 30 pekee na baada ya kuwaza kurudi kuichukua chaji ya simu yake alishangaa kulikosa gari lake.

Taarifa hiyo iliandikishwa katika kituo cha polisi cha Murang’a  huku uchunguzi ukiendelezwa.

About the author

admin

Leave a Comment