News

Mvua kubwa yatatiza Naivasha

Written by admin

N

 Zaidi ya familia 100  kule  Moi -Ndabi Mjini Naivasha zimeshauriwa kuhamia maeneo ya juu kufuatia mvua kubwa ambayo imenyesha eneo hilo usiku kucha.

Wengi wameadhiriwa na mafuriko hayo huku vyakula vilivyokuwa shambani pia vikiharibiwa baada ya mvua hiyo iliyonyesha maeneo ya juu ya Maella, Sakutiek na Viae.

Kulingana na mwakilishi wa wadi ya Maella Gathariki Kamanu, wanawake na watoto ni kati ya walioadhiriwa huku akiwataka wahisani wema kufika eneo hilo na kuwasaidia.

Haya yamejiri huku serikali ya kaunti ya Nakuru kupitia kwa katibu wa maswala ya dharura Ann Njenga ikifika eneo hilo na kutoa msaada wa chakula kwa familia zilizoadhirika.

SILAS MWITI

About the author

admin

Leave a Comment