News/Habari

Mwanaharakati: Wanaoishi na changamoto za ulemavu wapewe ajira na ujuzi

Watu wanaoishi na changamoto za ulemavu Marsabit.
Written by admin

Watu wanaoishi na changamoto za maumbile katika kaunti ndogo ya Bahati hapa Nakuru, wanaitaka serikali ya kaunti ya Nakuru kuwatengea nafasi zaidi za ajira.

 Jamii hiyo inasema wameshindwa kujiendeleza kimaisha kutokana na hali ngumu ya uchumi inayokabili taifa.

Akiongea na Sauti Ya Mwananchi katika eneo la Kabatini Angeline Akai  mtetezi wa haki za walemavu eneo bunge  la Bahati, amesema kuwa serikali ya kaunti ya Nakuru chini ya gavana Lee Kinyanjui, napaswa kuwahusisha walio na changamoto za kimaumbile kwenye kazi mbali mbali ambazo hutolewa na kaunti, ili kuwaondoa mitaani.

Akai amesema ni muhimu pia serikali ya kaunti iwafadhili  wanaoishi na changamoto za kimaumbile katika kusomea taaluma mbali mbali, ambazo zitawasaidia katika kujitegemea.

“Tungependa watu wenye ulemavu waajiriwe ili wajikimu kimaisha, lau sivyo wapatiwe ujuzi wa kujiajiri. Wakati wa walemavu kwenda kuwa omba omba mitaani umepata. Ili waweze kujiimarisha na kuimarisha uchumi wa Kenya, lazima wote wanaoishi na changamoto za maumbile wapewe ujuzi” Akai akasema.

About the author

admin

Leave a Comment