Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Mogotio Albert Mwaringa amewaonya vijana dhidi ya kutumika visivyofaa au kuzua vurugu na watu ambao wamejitokeza kuwania viti mbali mbali vya kisiasa.
Akihutubu huko Mogotio, Mwaringa alisema baadhi ya vijana wanatumika kufanya maandamano msimu huu wa siasa na hasa vijana wanaomiliki pikipiki za bodaboda.
Naibu huyo wa Kamishna alitoa wito huu wakati ambapo vijana wanazidi kubuni vikundi vya kuunga mkono wanasiasa fulani, huku wakitumia pikipiki zao kufanya misafara kwa wanasiasa wanaozuru maeneo yao.