Wakulima na wamiliki wa ardhi yenye utata ya Utheri wa Lari kule Mai Mahiu wanakadiria hasara kubwa baada ya vijana wanaoaminika kutoka kwa jamii moja eneo hilo kuvamia ardhi hiyo na kuharibu mimea ya Castor Plants yenye dhamani ya mamilioni ya pesa.
Mwenyekiti wa ardhi hyo Stephen Muriu amesema kuwa takriban ekari 30 zilizokuwa zimepandwa mimea hiyo ya bei kubwa zimeharibiwa na kikundi hicho huku umiliki wa ardhi hiyo ukiendelea kuzua utata.
Muriu aidha amesema kuwa tukio hilo limejiri miezi michache baada ya maafisa kutoka hazina ya CDf ya mji wa Naivasha kuvamiwa na vijana hao walipokuwa wamefika eneo hilo kukagua ujenzi wa kituo cha polisi.
Nao katibu wa shamba hilo Peter Njihia na mwekahazina wake James Gichengo wamemtaka waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I kufika eneo hilo na kutatua mzozo huo kwani tangia mzozo huo kuanza, watu kumi watu 10 wamepoteza maisha yao.
NA SILAS MWITI
Leave a Comment