Ann Kananu amekula kiapo cha kuwa gavana wa tatu wa kaunti ya Nairobi. Kananu ameapishwa katika ukumbi wa jumba la mikutano KICC.
Kananu alikuwa kaimu gavana wa kaunti ya Nairobi kuanzia mwezi December 2020 baada ya kubanduliwa kwa aliyekuwa gavana Mike Sonko.
Kiongozi huyo anakuwa gavana wa kwanza wa kike wa kaunti ya Nairobi na wa nne tangu ujio wa ugatuzi baada ya Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru,Charity Ngilu wa Kitui na marehemu Joyce Laboso.
Leave a Comment