News/Habari

NAIROBI: SHULE YAFUNGWA KUPISHA UCHUNGUZI WA MKASA WA MOTO

Mabegi ya wanafunzi wa shule ya akina dada ya Buruburu yakiwa nje ya bweni lililoteketea jana Okt 31, 2021. PICHA/MAUREEN KINYANJUI
Written by admin

Shule ya upili ya wasichana ya Buruburu imewaruhusu wanafunzi kuenda nyumbani kufuatia mkasa wa moto ambao uliteketeza bweni moja jana.

Hatua hiyo ilichukuliwa ili kupisha uchunguzi wa kina kuhusiana na mkasa huo ambao ulitokea mwendo wa saa kumi unusu jioni.

Usimamizi wa shule hiyo ulitoa ilaniĀ  kwamba hatua kali itachukuliwa dhidi ya mwanafunzi yeyote atakayepatika kuhusika na tukio hilo.

Kwa sasa wanafunzi 35 wanaendelea kupokea matibabu, 19 kati yao wakitibiwa katika hospitali ya Metropolitan huku wengine 16 wakihudumiwa katika hospitali ya Jamaa.

Hali ya afya ya wanafunzi 34 waliolazwa hospitalini ni imara ila mmoja wa wanafunzi ambao waliruka walipokuwa wanajaribu kuokoa maisha yao aliripotiwa kuvunjika mguu.

Bodi ya shule hiyo ilikutana na wazazi kuzungumzia tukio hilo ambalo liliibua hofu kote nchini.

About the author

admin

Leave a Comment