Wadau katika sekta ya uchukuzi mjini Nakuru wametaka serikali ya kaunti kuharakisha ujenzi wa kituo cha kisasa cha matatu mjini ili kuboresha utenda kazi.
Mwenyekiti wa muungano wa wenye matatu kati mwa bonde la ufa Stephen Muli alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kisasa katika eneo la Railways umekawia kukamilika.
Kulingana na Muli kujikokota kwa zoezi hilo nzima kumeathiri biashara akitaja maafisa wa utekelezaji kwenye serikali ya kaunti kuhusika na ukokotaji huo kwa madai kuwa wanazidi kupokea hongo kutoka kwa magari ambayo hayafuati sheria ili kuwapa fursa ya kuendelea kupakia abiria kusiko stahili.
Katibu wa muungano wa wafanyibiashara mjini Simon ole Nasieku kwa upande wake amekashifu wanasiasa katika kaunti hii kwa kukosa kuunda sera ambazo zinaelekeza na kuhakikisha mandhari yaliyo sawa na salama kwa wafanyibiashara.
Leave a Comment