News/Habari

NAKURU: Kifo kilichofungamanishwa na mapenzi

Written by admin

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 48 kwa jina Anita Njeri anaendelea kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Menengai Magharibi  kaunti ndogo ya Rongai, akishukiwa kutekekeza mauaji.

Akidhibitisha hayo, OCPD wa Rongai Richard Rotich, amesema mwanamke huyo anashukiwa kumuua Teresia Chakoko mmiliki wa klabu moja katika kituo cha kibiashara cha ol-Rongai usiku wa Jumamosi.

Rotich amesema uchunguzi unaonyesha kuwa wawili hao walikuwa wanazozania mwanaume mmoja.

Kulingana na Rotich, mwili wa marehemu ulipatikana chumbani ukiwa na majeraha, ila kunasubiriwa upasuaji kubaini chanzo cha kifo chake.

About the author

admin

Leave a Comment