News/Habari

NAKURU: MATUMIZI YA MOTO YAPIGWA STOP!!!

Written by admin

Chifu wa kata ya Rongai John Njagi, amewaonya wakaazi wa kata hiyo dhidi ya kutumia moto  wakati wa kutayarisha mashamba yao kwa upanzi.

Njagi, alisema Rongai iliathirika pakubwa na visa vya moto mwishoni  mwa mwaka jana na wananchi wanapaswa kuwa waangalifu ili kuepukana na visa kama hivyo msimu huu.

Aliongeza kuwa, utumizi wa moto kama mbinu ya kutayarisha mashamba ni hatari sio tu kwa wananchi bali pia kwa mazingira hususan majira haya ya kiangazi.

About the author

admin

Leave a Comment