Huzuni imetanda kule Moricho katika kaunti ndogo ya rongai, baada ya kijana mmoja kwa jina Bernard Kipkemoi Tanui mwenye umri wa miaka 30 kujitoa uhai kwa kujinyonga.
Akidhibitisha kisa hiki, chifu wa Moricho Moses Rotich, amesema kijana huyo amekuwa akiugua kwa mda, maradhi ambayo yamemsababishia msongamano wa mawazo.
Marehemu anaripotiwa kuijulisha familia yake kuwa ameshindwa kuendelea na maisha na anaonelea vyema ajitoe uhai.
Kijana huyo amepatikana mapema leo akiwa amejinyonga karibu na mto Molo.
Mwili wa marehemu umepelekwa kwenye makafani ya Kwa Jack mjini Nakuru.
Leave a Comment