Wanafunzi wa shule ya upili ya Molo Academy wametumwa nyumbani na shule hiyo kufungwa kwa mda usiojulikana baada ya maandamano ya usiku wa kiamkia leo yaliyosababisha polisi kuingilia kati.
Maandamano hayo yanasadikika kusababishwa na kukosekana mwafaka baina ya wazazi, washikadau wa elimu eneo hilo, usimamizi wa shule na watawala wa mkoa kwenye mkutano wa pamoja.
Leave a Comment