News/Habari

NAKURU: WANANCHI WAIPA SERIKALI MSAADA WA ARDHI

Written by admin

Wakaazi wa mtaa wa Makao wadi ya Kiamaina hapa Bahati, wamekabidhi kipande cha ardhi kwa serikali, wakitaka kujengewa kituo cha polisi ili kuimarisha usalama.

Kulingana nao, wamekuwa wakihangaishwa na kikundi cha vijana kinachojulikana kama confirmed, jambo ambalo limewafanya wengi wao kuhofia maisha yao.

Wameendelea kusema  kituo cha polisi kwenye eneo hili kitasaidia kurejesha usalama na kuleta mazingira mazuri ya kufanya biashara.

About the author

admin

Leave a Comment