News/Habari

NATEMBEYA: SIO MALISHO, WAPO WENYE HAJA KWENYE HOJA

Mshirikishi wa Bonde la ufa George Natembeya.
Written by admin

Mshirikishi wa kanda ya bonde la ufa George Natembeya amesema kuwa vita vya utovu wa usalama vinavyoshuhudiwa katika eneo la Laikipia havitokani na  malisho bali mizozo ya  mashamba na kuwa baadhi ya viongozi nchini wanahusishwa.

Natembeya, amesema watu wanane, wakiwemo polisi watatu, ndio wamepoteza maisha katika muda wa mwezi mmoja kutokana na vita vya kule Laikipia.

Wanauguza majeraha ni raia wanne na polisi wawili, Natembeya akikanusha taarifa kwamba  darasa liliteketezwa wakati oparesheni ya polisi ikiendelea.

About the author

admin

Leave a Comment