Gavana wa Kitui, Charity Ngilu amemkashifu Naibu wa Rais William Ruto huku akisema anatakiwa kujiuzulu kwa ofisi yake ya Harambee Annex kuhusishwa katika visa vya utapeli.
Kulingana na Ngilu, makamo wa rais ni sehemu ya urais na hivyo anatakiwa kuhakikisha kuwa mali ya wananchi na usalama wao unalindwa.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mnamo Jumapili, Februari 16, Ngilu alizua kuwa Ruto aliathiri usalama wa taifa hili kwa kuhusika katika zabuni feki ya kutoa vifaa vya kijeshi.
Gavana huyo alifichua kuwa sio mara ya kwanza Ruto kuhusishwa katika sakata za ulaghai. Alidai kwamba Stephen Ngei Musyoka, wa Makindu Motors, pia ni mwathiriwa ulaghai katika ofisi ya Ruto.
Matamshi ya Gavana huyo yalikujia siku moja tu baada ya Ruto kukiri alikutana na walaghai hao wa zabuni feki ya KSh 39.5 bilioni ya kusambaza vifaa vya kijeshi katika ofisi yake kwa muda wa dakika 23.
Ruto anashikilia kuwa hana makosa kuhusiana na sakata hiyo na yote ilikuwa njama ya wakinzani wake wa kisiasa ili kupaka jina lake tope.
Leave a Comment