News/Habari

NYANDARUA: AJALI YA MOTO YAMUANGAMIZA AJUZA!!

Written by admin

Wingu la simanzi limetanda katika Kijiji cha Kirimangai kule Kasuku kaunti ya Nyandarua baada ya ajuza (99) kuteketezwa na Moto kiasi Cha kutotambulika  leo alfajiri.

Kulingana na ripoti ya polisi, mabaki ya mwili wa ajuza huyo kwa jina Ruth Munyive Mwinde yalipelekwa  katika makafani ya hospitali ya J.M Kariuki huku uchunguzi wa kiini cha Moto huo ukianzishwa.

Familia
ya ajuza huyo ambayo imezungumza na kituo hiki kwa njia ya simu imesema   ukosefu wa maji katika eneo hilo ulifanya
juhudi  za kuuzima moto huo  zisifue dafu.

About the author

admin

Leave a Comment