Ukarabati wa barabara ya Maumau inayounganisha kaunti za Nyandarua, Murang’a na Nyeri umekubwa na changamoto kwani barabara hiyo inapitia katikati mwa msitu wa Aberdare.
Mhadisi Evans Kinyua anayesimamia ukarabati wa barabara ya Njabini- Kinyona alisema kuwa changamoto hiyo ya msitu imeathiri utendakazi pamoja na hali ya mvua tele.
Akikagua ujenzi wa barabara hiyo mratibu wa serikali katika mkoa wa Kati Wilfred Nyangwanga alisema kuwa serikali itasuluhisha changamoto iliyoko na kuhakikisha msitu umehifadhiwa kwa kupanda kiasi Cha miti itakayokatwa ili kuafikia asilimia 10 ya misitu nchini.
Leave a Comment