News/Habari

Nyandarua: Corona bungeni

Bunge la kaunti ya Nyandarua katika vikao vya awali/facebook.com
Written by admin

Bunge la kaunti ya Nyandarua limefungwa kwa mda wa siku kumi na nne kufuatia maambukizi ya virusi vya Corona katika bunge hilo.

Naibu spika wa bunge hilo, Zachary Njeru, amesema   hatua hiyo imechukuliwa ili kuzuia maambukizi zaidi ya wimbi la Delta Variant bungeni, shughuli za kamati zikitakiwa sasa kuendelezwa mitandaoni.

Aidha Njeru amewahimiza wawakilishi wadi pamoja na wafanyakazi katika bunge hilo kutumia mda huo wa siku kumi na nne kuchanjwa na kuwahamasisha wakazi wa kaunti ya hiyo kupokea chanjo.

About the author

admin

Leave a Comment