Bunge la kaunti ya Nyandarua limerejelea vikao vyake hii leo baada ya kuvisitisha kufuatia msambao wa ugonjwa wa Covid-19.
Bunge hilo lilikuwa limefungwa kwa takriban mwaka ili kuwapa nafasi wafanyakazi pamoja na wawakilishi wadi waliokuwa wameathirika na ugonjwa huo kupona.
Kuhusu suala la kucheleweshwa kwa mishahara ya wafanyakazi wa bunge hilo kwa mda wa miezi miwili, usimamizi wa bunge hilo umesema kuwa ni changamoto ambayo imesababishwa na kukawia kwa fedha kutoka kwa wizara wala si kutokana na migogoro ya uongozi Kati ya aliyekuwa spika wa bunge hilo Ndegwa Wahome na uongozi uliopo.
Leave a Comment