News/Habari

NYANDARUA: OPARESHENI MOJA SAFI SANA!

Written by admin

Maafisa wa polisi mjini Olkalou kaunti ya Nyandarua wamewapata kondoo 37 walioibwa kutoka Kijiji cha  Bahati eneo hilo la Olkalou.

Oparesheni ya kuwasaka kondoo hao iliyoongozwa na OCS wa Kituo Cha polisi Cha Olkalou ilifua dafu usiku wa kuamkia leo ila mshukiwa akatoweka.

Naibu OCPD wa Nyandarua ya Kati Brigitte Kanini alisema kuwa uchunguzi unaendelezwa huku mkewe mshukiwa huyo akitiwa mbaroni.

About the author

admin

Leave a Comment