Naibu Kamishna wa Nyandarua ya Kati Gideon Oyagi ametoa onyo kwa wazazi ambao watoto wao hawajajiunga na kidato cha kwanza kufikia Sasa.
Akizungumza na kituo hiki,Oyagi amesema kwamba ushirikiano na machifu wataanza mikakati ya kuwatambua wanafunzi ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza, na kuona wanafanya hivyo kama njia moja ya kuafikia asilimia mia moja ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza.
Haya yanajiri wakati ambapo wazazi wamekuwa wakilalamika kufuatia ukosefu wa karo na pia basari za kaunti huku wengi wakilalamikia ugumu wa maisha kutokana na janga la korona.
Leave a Comment