Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 48 kutoka Geta Bushi, Kipipiri Kaunti ya Nyandarua ameaga dunia baada ya kuteketea ndani ya nyumba yake.
Kulingana na chifu wa eneo hilo la Geta Maina Ng’anga Moto huo uliteketeza nyumba takribani 5 za mbao zilizoko katika soko la Geta mwendo wa saa nne usiku huku zingine nane zikibomolewa ili kuzuia Moto huo kusambaa.
Haya yanajiri baada ya moto kuteketeza majengo katika Soko hilo la Geta miezi miwili iliyopita na kusababisha hasara kubwa. Kinachosababisha mioto hiyo bado hakijabainika.
Leave a Comment