Maafisa wa polisi katika eneo la Olkalou kaunti ya Nyandarua wameendeleza juhudi za kukomesha pombe haramu katika eneo hilo ambapo wamemnasa mwanamme mmoja akiwa na katoni 75 za pombe ambayo haijaidhinishwa na mashirika ya KEBS wala KRA.
Kulingana na OCPD wa Nyandarua ya Kati Dahir Abdillahi pombe hiyo ina thamani ya shilingi 150,000 na aliwarai wakazi wa eneo hilo kuendelea kushirikiana na maafisa wa polisi kwa kutoa taarifa ili kukomeza uuzaji wa pombe ambazo hazijahalalishwa.
Leave a Comment