Wamiliki wa baa zaidi ya 1,800 katika Kaunti ya Nyandarua ambao leseni zao za kibiashara hazikuongezewa muda, wametakiwa kuuza pombe yao ya Shilingi milioni 100 kufikia leo jioni kabla ya biashara hizo kufungwa kesho.
Haya yanakuja baada ya Kamati ya Kudhibiti Mauzo ya Vileo kwenye Kaunti ya Nyandarua kukagua na kutoa upya leseni kwa baa 600 kati ya 900 ambayo wamiliki wao walituma maombi ili kuendelea kufanya biashara hiyo.
Kaunti hiyo ina baa 2,400 ila nyingi zimekuwa zikiendeleza biashara hiyo kiharamu bila kufuata sheria.
Wamiliki wa baa hizo pia walikataa kutuma maombi ya leseni mpya wakilalamikia masharti makali yaliyowekwa na kamati ya kaunti.
Mwenyekiti wa Muungano wa Wamiliki wa baa Kariu Ng’ang’a amekashifu kamati hiyo, akisema itakuwa vigumu kuuza pombe zote kufikia leo huku akiomba muda huo usongeshwe.
Leave a Comment