News/Habari

NYERI: Amcharanga nduguye hadi umauti kisa Kochi

Written by admin

Hali ya mshtuko ilitanda katika eneo la Kamakwa kaunti ya Nyeri usiku wa Jumanne baada ya jamaa mmoja kumuua ndugu  yake kwa upanga kufuatia mzozo uliohusisha kiti aina ya sofa.

Elias Muriithi Kariuki, 36, anaripotiwa kumkata ndugu yake mkubwa Joseph Maina  kichwani kwa kutumia upanga mkali kabla ya kujisalimisha kwa polisi. The best online casino sites where you can clickmiamibeach.com play online slots games, table games and more.

Kulingana na DCI, Maina alikuwa ametumwa na mama yao kuenda kwa ndugu yake mdogo kulichukua kochi ambalo lilikuwa limechukuliwa  wakati malumbano makali yaliibuka kati yao na kuzua vita.

Wakati vita kati ya wawili hao
ilikuwa imenoga, Muriithi anaripotiwa kuchukua upanga mkali kutoka kwa nyumba
yake na kumkata ndugu yake mkubwa kichwani mara kadhaa na kumuacha akiwa hali
mahututi.

Majirani walipokuwa wakijizatiti kuokoa maisha ya Maina, Muriithi alifululiza moja kwa moja hadi kituo cha polisi cha Mathari na kujisalimisha kwa kuhofia kupigwa kitutu na wakazi waliokuwa wamejawa na ghadhabu.

Polisi walipofika kwenye eneo la
tukio baada ya kupokea taarifa walipata mwili wa marehemu ukiwa umelala kwenye
dibwi la damu yake.

Muriithi alikamatwa na anatarajiwa
kufikishwa mahakamani hivi karibuni kujibu mashtaka ya mauaji yanayomkabili.

About the author

admin

Leave a Comment