Bingwa wa jumuiya ya madola katika mita mia 100,..Ferdinand Omanyala ndiye mwanamichezo bora wa mwezi Agosti katika tuzo za kila mwezi za chama cha wanabahari wa michezo nchini Kenya (S.J.A.K) kwa ushirikiano na kampuni ya vifaa ya LG.
Omanyala, ametuzwa ikiwa mara yake ya pili kutawazwa mshindi mwaka huu ,akimkaribia mchezaji Tenisi Angela Okutoyi ambaye anaongoza kwa kushinda tuzo tatu.
Afisa huyo wa Polisi aliye na umri wa miaka 26 ,aliandikisha historia kuwa Mkenya wa kwanza katika historia ya michezo ya jumuiya ya madola kushinda dhahabu ya mita mia 100 , baada ya miaka 60 tarehe tatu mwezi uliopita mjini Birmingham.
Kufuatia ushindi huo Omanyala alipokea mashine ya kufua nguo chapa ya L.G ya thamani ya shilingi laki moja na elfu tano.
Omanyala amemshinda nyota awa raga (Billy Odhiambo) ,bingwa wa jumuiya ya madola katika mita mia 800 Mary Moraa na Hellen Wawira aliyenyakua nishani ya shaba ya jumuiya ya madola ,na bingwa mara mbili wa Olimpiki na Dunia WA MITA elfu 1,500 Faith Kipyegon ,ili kutawazwa mshindi.
Wengine waliokuwa kwenye orodha hiyo ni mchezaji wa netiboli (Beatrice Bucho, Jackline Chepkoech) aliyeshinda dahabu ya mita elfu 3,000 kuruka maji na viunzi , (Faisal Aden) wa timu ya mpira wa kikapu ya (Equity) na bingwa wa dunia katika mita elfu 3,000 kuruka maji na viunzi kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 ,(Faith Cherotich).
Leave a Comment