RAIS mpya William Ruto ametangaza Jumanne kuteua majaji sita wa mahakama ya rufaa, waliokataliwa na mtangulizi wake.
Akihutubu katika uwanja wa Moi, Kasarani Nairobi baada ya yeye na naibu wake, Rigathi Gachagua kuapishwa rasmi kama Rais na Naibu Rais mtawalia, amesema atasimamia kuapishwa kwao kesho Jumatano.
Majaji sita ambao Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta alikataa kuwateua licha ya Tume ya Idara ya Mahakama (JSC) kuwapendekeza ni George Odunga, Aggrey Muchelule, Joel Ngugi na Weldon Korir, pamoja na hakimu mkuu Evans Makori na naibu msajili wa Mahakama Kuu Judith Omange.
Aidha sita hao ni miongoni mwa 40 waliopandishwa madaraka na JSC Juni 2021.
Isitoshe, Rais Kenyatta alikataa kuteua sita hao, licha ya amri ya Mahakama Kuu.
Rais huyo wa tano wa Jamhuri ya Kenya, vilevile ametangaza nyongeza ya mgao wa bajeti kwa idara ya mahakama.
Leave a Comment