News/Habari

Serikali yaahidi dawa huku 5 wakiangamia

Written by admin

Wakazi kutoka eneo la Kerio Valley kaunti ya Elgeyo Marakwet wanaishi kwa hofu baada ya watu 5 kuripotiwa kufariki hii leo  kutokana na mkurupuko wa ugonjwa wa Malaria.

 Kulingana na waziri wa afya na usafi katika kaunti hiyo Kiprono Chepkok, serikali inajisatiti kuona kuwa wamenunua dawa ikizingatiwa  kuwa kuna upungufu wa dawa katika shirika la usambazaji wa dawa ya KEMSA

 Mwalikishi wa wadi ya Emsoo John Yator kwa upande wake ameomba serikali ya kaunti hiyo kutafuta suluhu la kudumu ikizingatiwa kuwa wadi hiyo ni miongoni mwa maeneo ambayo yameathirika.

Haya yanjiri huku serikali ya kaunti hiyo ikikosa dawa ya kutibu ugonjwa huo.

About the author

admin

Leave a Comment