News

Serikali yaombwa kutangaza Kapedo kama kambi ya Askari jeshi

Written by admin

Mbunge wa Tiaty kwenye kaunti ya Baringo Wiiliam Kamket sasa anatoa wito kwa serikali kutangaza eneo la KAPEDO kuwa kambi ya askari jeshi,ili kumaliza mzozo na vita za mara baina ya jamii za Pokot na Turkana.

Akihutubu jana katika eneobunge lake wakati wa ziara yake kamishna mshirikishi wa ukanda wa bonde la ufa George Natembeya,Kamket anasema mizozo baina ya jamii za Turkana na Pokot imesababisha vifo vingi na hivyo serikali inafaa kuwaondoa wananchi katika eneohilo la Kapedo…

Huku akihimiza machifu wote kusaidia serikali kuwakamata wahalifu waliotekeleza mashambulizi ya Kapedo siku ya Jumatatu iliyopita ,nambapo askari mmoja na raia wawili waliuwawa baada ya gari lao kushambuliwa,Kamket pia amemhimiza bwana Natembeya kuwafuta kazi machifu wote ambao wanaishi nje ya lokesheni zao…

Bwana Natembeya alizuru eneohilo hiyo jana na kutangaza kwamba waliohusika katika mauaji ya askari ya siku ya Jumatatu ni sharti wakamatwe,na kushtakiwa.

About the author

admin

Leave a Comment