News/Habari

Shule zitakazotumika kama vituo vya kupigia kura kaunti za Kakamega na Mombasa kufungwa Agosti 29 na kufunguliwa Agosti 31

Waziri wa elimu Magoha
Written by admin

Waziri wa elimu profesa George Magoha amesema kwamba shule za kutwa katika kaunti za Kakamega na Mombasa pamoja na maeneo mengine ambayo uchaguzi uliahirishwa zitafungwa Agosti 29 na kufunguliwa Agosti 30 ili kupisha tume ya IEBC kutumia sehemu hizo kama vituo vya uchaguzi huo.

Magoha alisema kwamba shule za bweni hazitaathirika na mpango huo kwani wanafunzi watabaki katika mabweni wakati madarasa yatatumiwa kwa shuguli hiyo kwa siku moja na masomo kuendelea kama kawaida kuanzia kesho yake ambayo itakuwa Jumanne Agosti 30.

Alisema kwa sababu hawataki watoto kukosa masomo na kuharibu muda basi watoto watakaokuwa nje kwa hiyo siku moja ni wale wa shule za kutwa na wa shule za bweni watasalia katika mabweni.

Taarifa hii inakuja siku moja tu baada ya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutangaza kwamba chaguzi zote zilizoahirishwa zitafanyika Jumatatu Agosti 29.

About the author

admin

Leave a Comment