News/Habari

SHULENI: MWANZO WA TIBA

Written by admin

Wanafunzi sita wa shule ya wavulana ya Maranda katika kaunti ya Siaya wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo, baada ya kukamatwa kuhusiana na moto ulioteketeza bweni moja la shule hiyo usiku wa Jumapili.

Wanafunzi hao sita walinaswa kwenye kamera  za CCTV wakitembea kando ya bweni hilo wakati
liliposhika moto.

Mkurugenzi wa elimu katika kaunti hiyo Nelson Sifuna, alisema wanafunzi hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha kaunti ndogo ya Bondo ili kuhojiwa.

Alisema kwa bahati nzuri hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wakati wa kisa
hicho lakini shule hiyo imefungwa kwa muda usiojulikana ili kuwezesha
wasimamizi kukarabati bweni hilo lenye vitanda 178.

About the author

admin

Leave a Comment