MCA mmoja wa kaunti ya Siaya alikiri kupokea hongo kutoka kwa ofisi ya gavana wa kaunti hiyo ili kufungia jicho masuala ya ufisadi kwenye kaunti hiyo.
Kukiri kwa mwakilishi wadi ya Asembo Magharibi Ambrose Akuno kwamba alipokea hongo hiyo, kunajiri licha ya juhudi za spika George Okode kumtetea MCA huyo dhidi ya madai ya hongo wiki jana.
Okode wiki jana alikuwa amekanusha madai kwamba MCAs wa Siaya walipokea hongo ili kufunikia ripoti ya ubadhirifu wa shilingi milioni 600 katika kaunti hiyo.
Ripoti iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ilisema wawakilishi wadi hao walikuwa wamepokea kiasi cha shilingi 290,000/= kila mmoja kutoka kwa ofisi ya gavana wao.
Hata hivyo sasa Akuno anasema alipokezwa shilingi 150,000/=, akisema aligundua baadaye kwamba pesa hizo zilikuwa miongoni mwa zilizotolewa kwa wenzake kama hongo.
Leave a Comment