Gavana wa kaunti ya Elgeyo Marakwet Alex Tolgos amefutilia mbali habari inayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amejiuzulu.
Kulingana na taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari gavana Tolgos amewahakikishia wakazi wa kaunti hiyo kuwa hajachukua hatua kama hiyo, huku juhudi zikiendelea kumsaka aliyeandika barua hiyo kwa spika wa bunge la kaunti hiyo Philemon Sabulei.
Barua hiyo ilikuwa imeandikwa kuwa gavana Tolgos angependa kujiuzulu kwa sababu kadhaa ikiwemo afya yake, kutishiwa maisha na pia familia yake.
Leave a Comment