Hatimaye soko la wakulima la Nakuru litafunguliwa tena baada ya kufungwa kwa kipindi cha miezi mitatu na kupelekea wafanyibiashara wa soko hilo kuhamishwa hadi uga wa Afraha na serikali ya kaunti kama njia moja ya kuzuia maambukizi ya homa ya korona kufuatia kuzuka kwa janga hilo nchini.
Kwenye taarifa yake gavana wa kaunti ya Nakuru Lee Kinyanjui kwa vyombo vya habari ni kuwa soko hili litafunguliwa mnamo Septemba 13 na shughuli zake kuanza rasmi jumatatu ijayo tarehe kumi na nne mwezi huu.
Aidha, amedokeza kuwa serikali yake kupitia idara ya afya kwa umma itahakikisha kuwa wafanyibiashara hao wanazingatia kanuni za wiazra ya afya ili kuzuia maambukizi zaidi.
Uga wa Afraha Annex na ambao umekuwa ukitumika kama soko wakati wa kipindi cha Covid-19.
Leave a Comment