Mbunge wa Subukia Samuel Gachobe amewataka wakaazi kutojihusisha na siasa zisizo na mwelekeo na badala yake waendelee kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta.
Akiongea kwenye soko la Subukia Gachobe amesema kuwa, kama viongozi wataendelea kushirikiana na Rais pamoja na naibu wake, ili kuhakikisha kwamba wananchi wamefikiwa na maendeleo.
Aidha, amewataka wakaazi kuendelea kudumisha amani na umoja, na hata kutia bidii kwenye kazi zao, ili waweze kusonga mbele kimaendeleo.
Wakati uo huo mwakilishi wadi ya Kabazi Dkt Peter Mbae, amewataka vijana na wakaazi kwa jumla kujiunga na vyama vya ushirika (Saccos) ili waweze kujiinua.
Akiongea katika mkutano uliowaleta pamoja wakaazi na viongozi wa eneo la Subukia, Mbae amewataka wakaazi hasa vijana, kutumia mikopo na kujiimarisha kupitia biashara ndogo ndogo, kama njia moja ya kupigana na umaskini katika jamii.
Wakati huo huo, ameongeza kuwa kama viongozi wa eneo la Subukia, watahakikisha kwamba vijana wote wamesaidika kupitia miradi mbalimbali, ili kuwaepusha na masuala ya uhalifu.
Na Warukira Mwangi
Leave a Comment