Hali ya taharuki imetanda katika eneo la Kamacabi kule Tharaka Nithi baada ya wezi wa mifugo kuwavaamia na kuiba mamia ya mifugo.
Wezi hao waliokuwa zaidi ya 30, kulingana na wenyeji wa Kamacabi, walikuwa wamejihami kwa bunduki na kuvalia sare za kijeshi.
Kwa mujibu wa wakaazi, wezi hao wenye asili ya kisomali, walitoweka na mamia ya mifugo wakiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda ambao wanategemea kiuchumi haswa wakati kuna ukame.
Leave a Comment